Historia ya FADHWAAILUL AYTAAM GROUP
بسم الله الرحمن الرحيم Assalamu 'alaykum warahmatullahi wabarakatuh Historia ya fupi "FADHWAAILUL AYTAAM GROUP" ni Kikundi maalumu cha kiislamu kinachojihusisha na kuwasaidia mayatima , walemavu , wasiojiweza na wajane kinachoendeshwa kupitia mitandao ya kijamii kilianzishwa rasmi siku ya jumapili ya tarehe 09/12/2018 kupitia mtandao wa WhatsApp pekee kikiongozwa na viongozi wafuatao:- 1. Maulid Bin Swaleh (Mwenyekiti) 2. Kisandu Bin Kusolwa (Katibu) 3. Mariam Abdulrahman (M/hazina) 4. Abuubakari Saidi (Mratibu wa safari) Katika kipindi hicho kikundi kilikuwa katika kipindi kigumu sana hususani katika masuala ya kiuchumi pia katika nyoyo za watu ziamini ukweli kuhusu lengo la kikundi hakika kipindi hicho viongozi walijitolea muda wao na bundle(bando) zao ili waweze kuhamasisha jambo la kheri la kuwasaidia yatima, walemavu, wajane na wasiojiweza Kikundi kilikaa muda mrefu pasipokuwa na safari/ziara ya kikundi kutokana na mapato kuwa chini. Kikundi kilianza safari/ziara zak...